Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Biashara haramu ya duma

Maafisa wa kuhifadhi wanyama pori nchini Ethiopia wamesema kusafirishwa kinyume cha sheria kwa duma kutoka nchini humo kuelekea katika mataifa ya ghuba imeifikia kiwango cha kutia wasiwasi mkubwa.

Shirika la wanyama pori nchini Ethiopia limesema takriban duma wanne wanasafirishwa kutoka nchini humo kila mwezi kuelekea Saudi Arabia na katika mataifa mengine ya ghuba ambapo hufugwa kama wanyama wa nyumbani.

Duma mmoja anakadiriwa kugharimu kiasi kisichopungua dola mia tano Ethiopia, lakini wanapofika katika nchi za ghuba, huuzwa kwa takriban dola elfu kumi.Kila mwezi, Duma wapatao wanne huwa wanaibiwa nchini Ethiopia, Mamlaka ya wanyama pori Ethiopia(WCA).

Mkurugenzi wa mamlaka ya hifadhi ya wanyama pori anasema kuwa wenyeji huwa wanashiriki katika kuwakamata duma hao ili kujikimu kifedha.

Wenyeji huwa wanalipwa dola 310 mpaka dola 466 kwa kila duma.

Duma hawa huwa wanatoroshwa kwenda Hargeisa, mji mkuu wa Jamuhuri ya Somaliland na kusafirishwa kinyume na sheria mpaka Saudi Arabia na mataifa mengine ya kiarabu .

Huwezi kusikiliza tena
Duma 'awajulia hali' watalii kwenye gari Tanzania

Alisema pia duma hawa ambao wanauzwa katika soko lisilo halalali kwa kiasi cha fedha cha zaidi ya dola 10,000 kwa matajiri ambao wanapenda kufuga duma hawa nyumbani.

Bwana Pawlos aliongeza kusema kuwa duma hawa huwa wanatoroshwa kinyume na kuzwa sheria.

Mwezi Agosti, mwanaume mmoja wa Ethiopia alikamatwa Somaliland kwa kosa la utoroshaji wa duma.

"Tulifanikiwa kuwarejesha duma wetu Ethiopia na kumuweka katika kituo cha uokoaji," alisema bwana Pawlos.

  • Duma atembea kilomita 1,300 kutafuta 'mke'

Wiki iliyopita , kikosi cha usalama nchini Saudi Arabia kiliwakamata watu kadhaa kwa kujaribu kutorosha chui kaika nchi yao.

Hifadhi za wanyama pori wengi wanasema kuwa wanyama wengi wanakufa kutokana na biashara haramu ya usafirishaji wanyama, chui wengi wanatoroshwa katika nchi kama Somalia na Ethiopia.