Haki miliki ya picha EPA Image caption Rais wa Iran Hassan Rouhani (kulia) ametishia kuanza kutumia teknolojia yake ya nuklia

Iran imetangaza kuwa haitazingatia tena vikwazo vyovyote vilivyowekwa katika mpango wa nyuklia wa mwaka 2015 .

Katika taarifa yake, taifa hilo limesema kuwa halitaangalia kiwango gani ambacho kina uwezo wa kutumia katika utajiri wake kwa upande wa thamani ya utajiri, vifaa vitakavyotumika au utafiti na maendeleo.

Tangazo hilo limekuja baada ya baraza la mawaziri wa Iran kukutana Tehran .

Kumekuwa na mvutano mkubwa baada ya Marekani kumuua kiongozi wa jeshi wa Iran Qasem Soleimani huko Baghdad.

  • Jeshi la Marekani kufukuzwa Iraq
  • Kwa nini Marekani imeamua kumuua Qasem Soleiman sasa?

Taarifa kutoka Baghdad zinasema kuwa mazingira ya ubalozi wa Marekani yalikuwa yamelengwa kushambuliwa siku ya jumapili jioni .

Chanzo cha habari kimeiambia BBC kuwa kulikuwa mizunguko minne ya risasi ambazo zilikuwa hazipigwi upande wa ubalozi moja kwa moja.

Hakuna taarifa yeyote ya majeruhi iliyoripotiwa.

Nini kilichotokea Jumapili?

Mamia ya watu walijitokeza siku ya jumapili kupokea mwili wa shujaa wao Soleimani ambaye anatarajiwa kuzikwa siku ya jumanne.

Awali, mawaziri wa Iraq waliweka azimio la kutaka majesi yote ya kigeni kuondoka katika nchi yao mara baada ya kifo cha jenerali aliyeuwawa katika mapigano ya anga katika uwanja wa ndege wa Baghdad , siku ya Ijumaa.

Haki miliki ya picha AFP Image caption Melfu ya watu wamekusanyika nchini Iran, kupokea mwili wa jenerali aliyeuliwa

Wanajeshi wapatao 5,000 wa Marekani wapo Iraq kama sehemu ya makubaliano ya kimataifa kupambana dhidi ya kundi la kiislamu la Islamic state.

Ushirikiano umesitisha operesheni zake dhidi ya kundi la kiislamu (IS) nchini Iraq kabla ya kura kupigwa siku ya jumapili.

Rais Donald Trump amerudiarudia kutishia kuwa Marekani inaweza kufanya shambulio lingine Iran katika tukio la kulipiza kisasi kifo cha Soleimani, na imesema kuwa labda itafanya kufanya shambulio kwa namna mbaya zaidi.

Makubaliano ya mwaka 2015, ambayo Marekani ilifanya na Iran ni kama yametelekezwa tangu utawala wa Trump uingie madarakani na sasa umefikiwa mwisho wake.

Haki miliki ya picha Reuters

Wakati wa kampeni zake za urais na alipokuja kuwa rais, Donald Trump hakuacha kuona kuwa mipango ambayo aliiazisha mtangulizi wake rais Barack Obama kuwa sio mipango mizuri.

Licha ya kwamba mataifa mengine yote yaliyoweka saini mkataba huo kama Uingereza, Urusi, Ujerumani na Umoja wa Ulaya bado wanaamini kuwa ilikuwa ni mipango yenye tija.

Makubaliano yaliyojulikana kama JCPOA, yalihusisha mpango wa nuklia ya Iran kwa njia ya kuthibitiwa kwa namna nzuri kwa namna nzuri kwa kiwango kikubwa.

Lakini mafanikio makubwa yanaanza kuonekana katika mgogoro huu wa sasa - kuwa imesaidia kuzuia kuibuka vita ya haraka.

Kabla ya mkataba huo kusainiwa, kulikuwa na masuala mengi yaliyohusisha shughuli zilizofanywa na nuklia ya Tehran na kulikuwa na mianya ambayo ingeruhusu Israel au hata Marekani kushambulia nuklia ya Iran.

Pia unaweza kusoma zaidi
  • Trump: Iran haitaruhusiwa kumiliki silaha za nuklia
  • Iran: Mkataba wa nuklia hautajadiliwa tena
  • Trump aitaka Marekani kuboresha silaha za nuklia

Tangu Marekani ijitoe, Iran imefanikiwa kuvunja vikwazo muhimu vilivyowekwa katika mkataba huo wa JCPOA.

Na sasa inaonekana kuwa imeamua kuvipuuzia vikwazo vyote vya maubaliano.

Kile ambacho wanakizingatia sasa ni kile ambacho wanaamua kukifanya wao kama wao.

Kwa mfano kutumia kiwango cha 20% cha utajiri wake wa urani ? Jambo ambalo lingeweza kupunguza sana wakati ambao Tehran ingeweza kupata nyenzo zinazofaa kwa ajili ya kutengeneza mabomu.. swali ni je, sasa hivi Iran itaendelea kufuata utaratibu wa ukaguzi wa kimataifa?

Tumefikia kile ambacho utawala wa Trump ulitaka kifanyike tangu Mei 2018.

Lakini mataifa makubwa hawafurahishwi hata kidogo na mpango wa Iran kuvunja makubaliano ambayo waliyokubaliana, vilevile wameshtushwa sana na maamuzi yaliyofanywa na rais Trump ya kumuua kiongozi wa jeshi la Iran, maamuzi ambayo yanaweza kuifanya Marekani na Iran kuingia kwenye vita.

Msimamo wa Iran katika mpango wa nuklia ukoje?

Chini ya makubaliano ya mwaka 2015, Iran ilikubali kuweka kikomo cha matumizi ya nuklia na kuruhusu wakaguzi wa kimataifa kufanya hivyo kwa makubaliano kuwa mataifa hayo yataweza kuondoka vikwazo vya kiuchumi.

Haki miliki ya picha EPA

Rais wa Marekani Donald Trump alipuuzia makubaliano hayo mwaka 2018, na kusema kuwa inataka kuilazimisha Iran kufanya majadiliano mapya ili kuwa na mpango mpya ambao utaweza kuondoa vizuizi na uboresha silaha zake za nuklia.

Iran ilikataa kukubaliana katika mapendekezo hayo.

Imetangazwa kuwa makubaiano yaliyofikiwa mwishoni mwa wiki yalikuwa yanatarajiwa kabla ya kifo cha Soleimani.

Televisheni ya taifa ya Iran ilitangaza siku ya jumapili kuwa taifa halitazingatia tena vipingamizi vilivyowekwa katika mkataba wa mwaka 2015.

"Iran itaendelea kutumia utajiri wake wa nuklia bila vipingamizi vyovyote kwa kutumia teknolojia inayohitajika,"iliripotiwa.

Hata hivyo taarifa hiyo haikusema kuwa Iran inajiondoa katika makubaliano ambayo ilisaini na kuongeza kuwa taifa hilo litaendelea kushirikiana na mataifa yaliyoagizwa na Umoja wa matifa.

Iran ilisema kuwa iko tayari kwenda na kile kilichokubalika awali kama itaweza kunufaika na makubaliano hayo.