Mamlaka nchini China pamoja wa wataalamu wa matibabu wako mbioni kutafuta chimbuko la mlipuko unaoendelea wa coronavirus. Ikiwa ni pamoja na utambuzi wa binadamu wa kwanza aliyepata ugonjwa wa corona. 

Uchunguzi wa kesi hiyo itasaidia kueleza jinsi binadamu wa atatumika kumueleza.

  • Jinsi ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona

Kesi hiyo pia itatumika kueleza jinsi binadamu wa kwanza alivyoambukizwa virusi ama mlipuko waugonjwa wa bakteria.

Uchunguzi wa hali juu wa mfumo wa jeni sasa unawawezesha wataalamu kugundua chimbuko la virusu kupitia wale walioambukizwa. 

Kupitia uchunguzi wa pamoja, wanasayansi wanaweza kubaini watu wa kwanza ambao huenda walisambaza ugonjwa na  hivyo kusababisha mlipuko.

Kuwatambua watu hao kunaweza kusaidia kujibu maswali muhimu kuhusu jinsi, lini na kwanini ilianza.

Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Soko la samaki la Huanan lililohusishwa na visa vya awali vya maambukizi ya coronavirus limefungwa

Hii inaweza kuwakinga watu zaidi dhidi ya maambukizi kwa wakati huu na magonjwa mengine ya mlipuko siku zijazo.

Lakini je tunamjua mgonjwa wa mlipuko wa Covid-19 coronavirus ulionza China?Kwa kifupi jibu ni - la.

Mamlaka ya China awali iliripoti kisa cha kwanza cha cha coronavirus kilikuwa Disemba 31 na visa vingi vilionesha dalili zinazokaribiana na  homa ya mapafu - ambavyo moja kwa moja vilihusishwa na vyakula vya baharini na soko ya nyama katika mji wa Wuhan, ulipo mkoa wa Hubei.

  • Je juhudi za kutafuta chanjo ya coronavirus zimefika wapi?
  • Jinsi ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona
  • Janga hili la corona litaisha lini?

Eneo hilo ni chimbuko la mlipuko wa corona, huku karibu 82% ya visa zaidi ya 75,000-vikiripotiwa China kufikia sasa na vingine vinavyoripotiwa kote duniani. 

Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins. (Soma zaidi jinsi ulimwengu unavyopambana na vita dhidi ya coronavirus.)

Hata hivyo uchunguzi uliyofanywa na watafiti wa Kichina na ambao ulichapishwa katika jarida la matibabu la Lancet, unadai kuwa mtu wa kwanza alipatilana na Covid-19, Disemba 1 2019 (mapema zaidi) na kwamba mtu huyo "hakukaribiana" soko la Huanan linalouza vyakula vya baharini kwa bei ya jumla.

Huwezi kusikiliza tena
Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?

Wu Wenjuan, daktari wa cheo cha juu hospitali ya Wuhan ya Jinyintan na mmoja wa wachunguzi katika utafiti huo, ameambia idhaa ya Kichina ya BBC kwamba mtu wa kwanza kupatikana na corona, alikuwa mwanamume mzee akiugua ugonjwa Alzheimer.

"Aliishi (mgonjjwa huyo) karibu na soko hilo na kwakua ni mgonjwa hakutoka nje ya nyumba," Wu Wenjuan alisema.Pia aliongeza kuwa watu wengine watatu walipatikana na dalili siku zilizofuata na wawili kati yao hawakufika Huanan.

Watafiti pia walibaini kuwa watu 27 kati ya wagonjwa 41 waliolazwa hospitali katika awamu ya kwanza ya mlipuko wa ugonjwa walitangamana na watu katika soko hilo.

Watafiti pia walibaini kuwa watu 27 kati ya wagonjwa 41 waliolazwa hospitali katika awamu ya kwanza ya mlipuko wa ugonjwa walitangamana na watu katika soko hilo.Lancet, Utafiti wa kimatibabu

Hatahivyo, watafiti waligundua kuwa watu 27 kati ya wagonjwa 41 waliokuwa wamelazwa hospitali katika awamu ya kwanza ya mlipuko corona "waliwahi kufika katika soko la samaki la Huanan".

Matokeo ya uchunguzi wa awali unaashiria kuwa maambukizi yalianza kusambaa kutoka soko hilo na huenda ilitokana na wanyama kabla ya kumuingia binadamu kabla ya maambukizi kuwa kati ya binadamu, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Je mwanadamu anaweza kusababisha mlipuko wa ugonjwa?

Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola uliokumba Afrika magharibi kati ya mwaka 2014 na 2016 mlipuko uligunduliwa kwanza 1976.

Uliwaua zaidi ya watu 11,000 na wengine zaidi ya 28,000,kupata maambukizi kulingana na WHO.

Mlipuko huo uliendelea kwa miaka miwili ana ulisambaa hadi mataifa 10, hususan barani Afrika japo visa vya vingine wiliripotiwa Marekani, Uhispania, Uingereza na Italia.

Wanasayansi walafikiana kuwa mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola ulitokana na mtu mmoja - mtoto wa miaka miwili kutoka Guinea - ambaye huenda alipata maaambukizi kwa kucheza karibu na mti uliokuwa makazi ya popo.